Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Mbwana Samatta kaweka rekodi mpya katika historia yake ya soka

Usiku wa August 25 nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ambaye anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji, jina lake lilirudi tena kwenye headlines kufuatia ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Lokomotiva Zagreb walioupata wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminas Arena. Katika ushindi huo wa goli 2-0 walioupata KRC Genk katika michuano ya kuwania kucheza hatua ya Makundi ya Europa League unawawezesha kufuzu hatua hiyo moja kwa moja kutokana na mchezo wao wa kwanza dhidi ya Lokomotiva walitoka sare ya goli 2-2.Samatta anaiwezesha Genk  kufuzu hatua ya makundi kwa mafanikio kutokana na kufunga goli la kwanza dakika ya 2 na baadae mjamaica Leon Bailey akafunga goli la pili, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Samatta kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Europa League.Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment