Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Wataalamu wazungumzia mihogo mibichi, nazi zinazouzwa na wakinamama DSM

 


Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya August 20 2016 ni hii kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Miujiza mihogo mibichi, Mbata kwa wanaume’
Gazeti la Nipashe limeripoti kuwa uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebainisha kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na akina mama jiini Dar es salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zink na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambatana cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.
Mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es salaam aliiambia Nipashe……..>>>’Vyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya akina baba, vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarishha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenza wao‘ 
Ofisa utafiti wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitishwa kitaalam kuwa husaidia kuimarisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayotokana hasa na Zinc.
Alisema kwa sababu hiyo ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es salaam na kwengineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa akina mama.  
SOURCE: NIPASHE
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment