Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Asilimia 60 wanaougua saratani wanatoka Mwanza

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori ambayo imeandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii ya kwenye gazeti la Mwananchi yenye kichwa cha Habari ‘Asilimia 60 wanaougua saratani wanatoka Mwanza
Gazeti hilo la Mwananchi limeripoti kuwa asilimia 60 ya watanzania wanaougua ugonjwa wa saratani nchini wanatoka mikoa ya kanda ya ziwa hasa katika mikoa Mkoa wa Mwanza. Hayo yalibainishwa na daktari wa magonjwa ya saratani wa hospitali ya Sekou Toure, Nestory Masalu wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alitaja sababu zinazochangia ugonjwa huo kuwa ni uwapo wa ziwa Victoria ambalo husababisha watu wengi kuugua kichocho, uchimbaji wa madini na shughuli za kilimo. Hata hivyo alisema wataalamu wa afya wanashindwa kukabiliana na tatizo hilo kutokana na ukosefu wa vifaa tiba kama RMI na st Scanza za kumpima mgonjwa kabla ya kumtibu 
>>>’kipimo kimoja hugharimu 300,000 kwa mtu mmoja, hai hiyo husababisha wagonjwa kupewa rufaa kwenda hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam’;-Nestory Masalu
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Kien Mteta alisema wanaupungufu wa vifaa hivyo na kuna vifaa vya kupimia saratani walivyopatiwa msaada tangu mwaka jana, lakini wamesema wamekosa fedha kwa ajili ya kuvifunga.
Dk Mteta alisema vifaa  hivyo viligharimu umla ya bilioni 6…..>>>’kufunga mashine moja zinahitajika bilioni 1 na hapa kwetu tunatakiwa kufunga mashine mbili ili ziweze kusaidia kupunguza wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda Dar es salaam’
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment