Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Balotelli aonyesha umwamba wake Ufaransa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia ambaye alitolewa bure na klabu ya Liverpool ya England kwenda klabu ya Nice ya Ufaransa Mario Balotelli, amerudi kwenye headlines baada ya maisha magumu ndani ya Anfield na AC Milan ya Italia alipokuwa anacheza kwa mkopo akitokea Liverpool.

Balotelli ambaye kajiunga na Nice akitolewa bure baada ya vilabu kadhaa kutoonesha imani ya kumuamini staa huyo, amefanikiwa kupachika magoli mawili katika ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Olympique Marsella, Balotelli alitumia dakika 7 za mwanzo kuiandikia Nice goli la kwanza kwa mkwaju wa penati na dakika ya 78 alipachika goli la pili lilifanya wawe sawa na Marsella waliokuwa tayari wamewafunga goli mbili.


Goli la tatu la Nice lililowapa point tatu na kuwafanya wapande hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa kwa kufikisha jumla ya point 10, lilifungwa na Wylan Cyprien dakika ya 88, wakati magoli ya Marsella yalifungwa na Thauvin dakika ya 14 na Gomis kwa penati dakika ya 72.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment