Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

‘CUF wabanwa kumtema Prof. Lipumba’Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori ambayo imeandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii ya kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha Habari ‘Maalim abanwa kumtema Lipumba’

Habari hiyo katika gazeti la Nipashe imeelza kuwa ofisi ya msajili wa vyama vyama vya siasa imemuandikia barua katibu mkuu wa chama cha wanachi CUF MaalimSeif Sharif Hamad ikimtaka kujibu malalamiko ya aliyekuwaa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba.
Aidha ofisi hiyo imeutaka uongozi wa chama hicho kueleza hatua ulizozipitia hadi kufikia uamuzi wa kumvua uenyekiti na kumsimamisha uanachama Prof Lipumba.
Ofisi hiyo imeupa uongozi wa CUF hadi kesho saa tisa na nusu alasiri kuhakakikisha imejibu barua hiyo iliyouandikia.
August 29 prof Lipumba aliwasilisha malalamiko kwenye ofisi hiyo akipinga kuvuliwa uenyekiti na kusimamishwa uanachama wa CUF.
Katika mahojiano na Nipashe jijini Dar es salaam Jana mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Monica Laurent alisema barua hiyo iliyoandikwa kwenda kwa chama hicho August 29 mwaka huu baada ya Prof Lipumba kuwasilisha barua siku hiyo akipinga kung’olewa kwa nafasi yake kwa madai kuw ataratibu hazikufuatwa.
Monica alisema ofisi hiyo haingilii masuala ya ndani ya vyama vya siasalakini vyama vinatakiwa kufuata taratibu, kanuni na katiba zake katika kujiendesha na kufanya uamuzi kwa masuala mbalimbali.
Source: Nipashe

Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment