Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Timu za Uingereza zafunika kwa Usajili Ghali zaidi


Vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza vimetumia zaidi ya paundi milioni 155 kufanya usajili kwenye kipindi cha majira ya joto, harakati zilizshuhudia timu hizo zikitumia paundi bilioni 1.165.Mpaka kufikia usiku wakati dirisha la usajili likifungwa, vilabu mbalimbali vilikuwa vimeshatumia paundi ya Uingereza bilioni 1.005, kiasi kinachopiku paundi milioni 870 zilizotumiwa na vilabu hivyo msimu wa mwaka jana.
Katika usajili huo, zaidi ya timu 13 ambazo zinashiriki Premier League vilivunja rekodi zao binafsi ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha lufanya usajili.
Vilabu 20 vya ligi kuu vimenufaika na ufadhili wa haki za televisheni kurusha matangazo, ambapo kiasi cha paundi bilioni 5.1 zimetumika kudhamini ligi ya msimu huu.
Vilabu viwili vya jiji la Manchester, vimetumia zaidi ya paundi milioni 150 kwenye dirisha la usajili msimu huu.
Manchester United chini ya kocha Jose Mourinho, walimsajili mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Paul Pogba kwa dauni la paundi milioni 89.
Klabu hiyo pia ilimsajili Muarmenia, Henrikh Mkhitaryan na mlinzi wa kati wa Ivory Coast Eric Bailly wote kwa pamoja kwa dau la paundi la milioni 30.
Manchester City wenyewe chini yua kocha wao mpya Pep Guardiola, walimsajili kiungo Leroy Saen kutoka Schalke kwa dauni la paundi milioni 37, na kuilipa klabu ya Everton kiasi cha paundi milioni 47.5 kumsajili beki wa kati wa Uingereza, John Stones.
Katika juhudi za kutaka kurejea kwenye hadhi ya ligi kuu, matajiri wa London klabu ya Chelsea, ilitumia kiasi cha paundi milioni 120, ikiwemo paundi milioni 34 kumsajili beki wa kati Mbrazil David Luiz akitokea PSG ya Ufaransa, ambapo pia imetumia paundi milioni 33 kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji, Michy Batshuayi kutokea Marseille.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment