Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

VIDEO: Mali za Freeman Mbowe zilivyotolewa nje ya jengo kisa deni la Bilioni

Kituo cha TV cha Channel Ten kimeripoti kwamba September 1 2016 shirika la nyumba la taifa NHC limevamia na kuondoa vifaa katika chumba cha habari cha gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mbowe Hotels chini ya Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Kampuni ya udalali ikishirikiana na NHC ilitoa vifaa hivyo nje huku Wafanyakazi wa ofisi hiyo wakiwa kwenye hali ya kushangazwa ambapo meneja wa kitengo cha kukusanya madeni NHC alisema taratibu zote zilifatwa na Mbowe Hotels walishapewa notice sababu Mbowe anadaiwa BILIONI 1.72
Kampuni ya udalali iliyosimamia hilo zoezi imesema baada ya kuvitoa vifaa hivyo nje vikishachukuliwa kwa maelekezo ya NHC baada ya wiki mbili mmiliki asipolipa deni vitauzwa.
Ilisemekana Mbowe Hotels anao umiliki wa asilimia 75 ya jengo hilo lakini shirika la nyumba la taifa (NHC) limesema umiliki huo ulishafutwa,
 unaweza kutazama hii video hapa chini kutazama ilivyokua.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment