Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Clinton na Trump 'kukwaruzana' katika mjadala wa pili


Image result for clinton vs trumpImage caption Trump na Clinton kukabiliana kwa mara ya pili
Wagombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump watasimama mbele ya jukwaa mjini Las Vegas baadaye kwa mjadala wa mwisho katika kile kinachoonekana kuwa kinyang'anyiro kikali cha urais.
Kura ya maoni inaonyesha kuwa Trump anaendelea kupoteza umaarufu wake baada ya kukabiliwa na madai ya kuwanyanyasa kingono wanawake.
Lakini Bi Clinton bado hana umaarufu mkubwa miongni mwa wapiga kura wa Marekani na amekabiliwa na vichwa vibaya vya habari kuhusu utumizi wa barua pepe za kibinafsi.
Wamarekani wengi watapiga kura Novemba 8.
Mamilioni ya watu wanatarajiwa kuutazama mjadala huo katika chuo kikuu cha Las Vegas ,mjini Nevada,ambao utaongozwa na mwandishi wa habari wa Fox News Chris Wallace.
Wagombea hao watajadili maswala sita ikiwemo deni la kitaifa,afya,faida za kijamii,uhamiaji,uchumi,mahakama ya juu,maswala ya kigeni na hali ya afya yao kuwa rais.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment