Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Hizi ndizo nchi hatari zaidi kutembea na kuendesha baiskeli

49% ya watu wanaofariki dunia katika ajali za barabarani ni wale wanaotembea, na kuendesha baiskeliImage copyright DAILY NATION

Malawi, Kenya, na Afrika kusini ndio nchi hatari zaidi kutembea kwa miguu na kuendesha baiskeli, utafiti wa Umoja wa mataifa kuhusu ajali za barabarani unasema.

Kati ya watu milioni 1.3 wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, 49% ni watu wanaotembea, waendesha baiskeli na pikipiki, shirika la mazingira la Umoja wa mataifa UNEP linasema.
Hizi ndizo takwimu za watu waliokufa wakitembea au wanapoendesha baiskeli katika ajali za barabarani:
  • Malawi: 49% wanaotembea, 14-17% wanaoendesha baiskeli
  • Kenya: 47% wanaotembea, 14% wanaoendesha baiskeli
  • Afrika kusini: 50% wanaotembea, 3% wanaoendesha baiskeli.
UNEP linasema uwekezaji wa dharura unahitajika kuimarisha miundo mbinu ya kutembea na kuendesha baiskeli ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

Ripoti ya utafiti huo wa UNEP iliyopewa jina 'Global Outlook on Walking and Cycling', inaeleza kuwa ukosefu wa uwekezaji katika kuhakikisha watu wanatembea na kuendesha baiskeli salama ndiyo unaochangia vifo vya mamilioni ya watu na kupuuza nafasi nzuri ya kuchangia katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment