Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Idadi ya wanyama yapungua kwa asilimia 60

Idadi ya wanyama pori na waishio majini imepungua kwa asilimia 60 tangu mwaka 1970 kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu. Hayo yameelezwa katika ripoti mpya ya shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira. Ripoti ya WWF iliyochapishwa leo Alhamis, ikijumuisha vipimo kwa kutumia data za shirika linalojihusisha na masuala ya wanyama la jijini London nchini Uingereza, ili kuangalia maisha ya wanyama katika sehemu mbalimbali duniani, imeonyesha kuwa idadi yao imepungua kwa asilimia 58  na kuwa kama hali hii itaendelea ifikapo mwaka 2020 idadi inakadiriwa kupungua zaidi na kufikia asilimia 67
Kupungua huku ni ishara nyingine kuwa wanadamu na shughuli mbalimbali wanazofanya ni moja kati ya mambo ambayo yanachangia mabadiliko duniani, huku ripoti hiyo ikiyataja mambo makuu matano ambayo yanachangia kupungua kwa wanyama kuwa ni pamoja na kupotea kwa makaazi, kuathiriwa na uchafuzi wa hali ya hewa, uvamizi wa viumbe wengine pamoja na magonjwa
Harakati mbalimbali za wahifadhi zinaonekana kuwa na matokeo duni kwa kuwa inaonesha kuwa kupungua kwa idadi ya wanyama duniani imepungua zaidi ya miaka miwili iliyopita ambapo shirika hilo lilikadiria kuwepo upungufu wa asilimia 52 ikilinganishwa na wanyama waliokuwepo mwaka 2010.
Mkurugenzi mkuu wa WWF Marco Lambertini amesema katika wakati huu wanyama wanapotea kwa kiwango ambacho hakikuwahi kushuhudiwa kabla
Utekelezaji mikataba ya kimataifa kusaidia
Huku Mkurugenzi wa sayansi kutoka shirika la wanyama jijini London Uingereza anasema ripoti hii inapaswa kuhamasisha mwamko wa juhudi kubwa kuzuia kutoweka kwa wanyama wa mwituni.
Inasisitizwa kuwa kuendela kuongezeka kwa idadi ya binadamu kunabaki kuwa kitisho kwa uhai wa wanyama duniani kwa kuwa maeneo mengi ambayo wanyama wamekuwa wakiishi hubadilishwa na kuwa mashamba na miji
Njia mojawapo ya kueleta matumaini ni makubaliano ambayo yalifikiwa na nchi karibu 200 juu ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, hii inaweza kusaidia katika kulinda misitu, kupunguza kuongezeka kwa majangwa na kudhibiti uchafuzi wa bahari unaotokana na kutengenezwa kwa hewa inayoathiri mazingira.
Mpango wa Umoja wa mataifa wa maendeleo endelevu wa mwaka 2015, unaolenga kukomesha umasikini kwa kuwa na sera ambazo zinahakikisha usalama wa mazingira ifikapo mwaka 2030, pia unatajwa unaweza kusaidia juhudi za kuokoa wanyama ikiwa utatekelezwa vizuri.
Mwandishi: Celina Mwakabwale/AFP/Reuters
Mhariri: Gakuba Daniel
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment