Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Je umewahi kukutana na matapeli wa aina hii?


Image result for some one cryingWakuu heshima zenu

Tahadhari kwa hizi namba tajwa hapo juu.

Siku ya Jumatano tarehe 19/10/2016 saa 3 asubuhi alinipigia bwana mmoja anajiita Samweli (0787-332977) akanitaja kwa jina nilosajili kwenye line yangu ya airtel na kuniuliza leo hujaenda kazini? Nikajibu ndiyo nipo home, akasema mimi naitwa Samweli(Mkurungezi wa kampuni nipo Dodoma) naomba uende AICC Hospital utamkuta Dr Shabani(0689-694153) mwambie Samweli ameniomba nisimamie mzigo wake wa dawa boxes 40 akataja jina gumu la dawa silikumbuki vizuri kila box shilingi 400,000 x 40 = 16,000,000.

Kuna mzungu anatokea KIA nakutumia no yake mara moja atakupigia mwambie wewe ni mwakilishi wa Kampuni na atakukabidhi million 24 cash, million 16 utalipa AICC na million 8 ni faida tutagawana mimi, mhasibu wangu na wewe, nikamjibu sawa. Baada ya muda mfupi akanipigia huyo Shabani A.K.A dr akaniuliza wewe ndiyo mwakilishi wa Samweli? Nikamjibu ndiyo. Mwambie wakaguzi wa TRA wanataka 480,000 cash bila mhuri wa TRA mzungu atakataa, nikamjibu kuwa ongea naye mimi nimeambiwa kusimamia kupaki mzigo (alipotaja hiyo hela nikaanza kushituka kuwa hapa kuna jambo). Baada ya muda Samweli akapiga cm akaniambia nimeongea na dr anataka 480,000 cash, akajifanya analalamika vibaya sana nikamwambia million 8 kutoa lakini 480,000 baki 7,520,000 mbona ni faida kubwa sana? Akasema isiwe tabu hapa mfukoni nina 280,000 naomba uniongezee laki 2 nikamwambia isiwe tatizo tuma hiyo 280,000 kwenye airtel money yangu nitaongezea hiyo laki 2 akasema sawa.

Baada ya kama dak 5 Shaban (dr) akapiga akasema Samweli amenitumia 280,000 amesema laki 2 unatoa wewe nikamjibu ni kweli natoa mimi lakini nipe dak 20 tu, baada ya dak 15 nikampigia nikamwambia nipo hapa getini japo sikuwa getini njoo unipokee au nielekeze ofisini kwako nipo na hela. Akasema ukiingia mlinzi atashituka nikamjibu mbona watu wengi wanaingia hashituki kwani anajua nakuja kufanya nini na wakati mimi nakuja kuonana na dr wangu? Wewe tuma kwenye simu nikamwambia poa ngoja niende airtel money town, Arusha airtel money ni za shida nyingi ni m-pesa akaniambia fanya haraka naandaa mzigo nije nao hotelini atapofikia mzungu na mhasibu wenu. Baada ya dak kama 5 mzungu feki(0787-407501) akapiga akaniambia anapata supu karibu na Golden Rose wapo na mhasibu wa kampuni lakini anavyoongea kimombo nikajua huyu ni tapeli, nikamwambia nakuja hapo nikufuate akakataa akasema anatafuta hoteli ya kulala na kupokelea mzigo.

Baada ya muda kidogo akanipigia Samweli (mkurugenzi feki) akaniuliza unafanya kazi gani? Nikamwambia nipo Monduli kambini akakata simu nikapiga hakupokea tena mpaka leo.

Hawajamaa ni matapeli wazoefu ukikurupuka unaenda na maji, maswali nilijiuliza inakuwaje mtu ambaye unamjua umuulize unafanya kazi gani? Kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni dr anashindwaje kukuamini 480,000 wakati mnafanya biashara ya mamilioni? Maswali ni mengi sana siwezi kuandika yote.

Hawajamaa wamesajili majina yale ambayo wanayatumia kutapeli lakini ukituma pesa hutakaa uwapate na wanaomba hela kidogo iliusishituke. Tuwe makini jamani nimeona ni wafahamishe msije mkatapeliwa na sijui na wanazitoa wapi no za simu za watu pamoja na kutaja eneo ulipo, kama hawashirikiani na watu wa customer care basi wanashirikiana na watu wa karibu yako.

Tusikimbilie hela za haraka unaweza kutapeliwa kirahisi sana.

Nilichelewa kuirusha/post kutokana kuwa na majukumu mengine nilikuwa sijapata muda wa kuichapa.

Jamani mimi siyo mwandishi wa habari kwa hiyo mapungufu mtanisamehe japo lengo langu ni tahadhari kwa wadau wasijitapeliwa.

Asanteni.

Aliyasema hayo jamaa mmoja kupitia mtandao wa jamii forum
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment