Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif amesema kuna njama za kumkamata na kumpulizia sumu itakayomuua


Image result for maalim seif 
 
Zanzibar. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuna njama za kumkamata na kumpulizia sumu itakayomuua taratibu.

Maalim Seif aliyezaliwa Oktoba 22, 1943 katika Kijiji cha Nyali wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, amesema hayo wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mwanasiasa huyo mkongwe ametoa tuhuma hizo juzi mbele ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Baraza Kuu, viongozi, watendaji na wafuasi wa CUF.

“Kwa taarifa za kuaminika, zipo njama za kunikamata, wanipeleke Dar es Salaam, kama walivyowafanyia masheikh. Waniweke katika chumba maalumu kidogo, kisha wanipulizie dawa hatimaye afya yangu izoroteshe afya taratibu na mwishowe nifariki dunia,” amedai Maalim Seif bila ya kutaja wanaotaka kumkamata.

Chanzo: Mwananchi
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment