Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ligi kuu kuendelea leo tenaLigi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itaendelea leo Oktoba 29,, 2016 kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili—michezo yote ikiwa ni ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa kwanza.
simba-vs-african-sports_55x7c0xbufr51ez19ifiigozj
Leo itakuwa ni zamu ya Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Jumapili Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment