Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Lindi atumbuliwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa,amemsimamisha kazi mkurugenzi wa mamlaka ya maji Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander, kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa kituo cha kuzalisha maji katika Manispaa ya hiyo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa malekezo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexanda muda mfupi kabla ya kumsimamisha kazi kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi akiwa kwenye ziara yake mkoani humo jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa malekezo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexanda muda mfupi kabla ya kumsimamisha kazi kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi akiwa kwenye ziara yake mkoani humo jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea mradi wa maji wa Ng’apa, ambapo aliagiza nafasi hiyo ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa Sengulo.
“Kamanda wa Takukuru fanya mapitio ya kina ya mshahara wake, yeye anasema analipwa mimi najua analipwa na Luwasa. Angalia kazi aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa,” alisisitiza waziri mkuu katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi yake jana.
“Huyu nimemuita mimi aje huku, hadi jana alikuwa Dar es Salaam,” alieleza Majaliwa.
Mkurugenzi huyo alipoulizwa sababu za kutokuwepo ofisini kwake kwa muda mrefu alisema kwamba alikuwa Dar es Salaam akiandika maombi ya fedha kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo.
“Unatumia siku ngapi kuandika proposal, msomi unatumia mwezi mzima kuandika proposal na unakaa Dar es Salaam hata Katibu Mkuu wako hajui na huko unajilipa posho tu! Tena baada ya kulipwa shilingi 120,000 kwa siku wewe unajilipa shilingi 150,000. Hatuwezi kuvumilia hali hii,” alisema.
Waziri Mkuu alisema serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi wanapata shida huku watendaji waliopewa dhamana ya kuwatumikia, hawaonekani kwenye vituo vyao vya kazi.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment