Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Makonda awapa siku 14 halmashauri za jiji la Dar kuwapa maeneo machinga

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa agizo kwa wafanyabiasara ndogondogo maarufu kama (machinga) wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara kuondoka na kwenda katika maeneo rasmi waliyopangiwa kufanya shughuli zao.
1-7
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa ongezeko la machinga barabarani limesababisha baadhi ya wananchi kulalamika uporaji kuongeza.
Makonda amesema kuwa, kurudi kwa wamachinga hao  kumesababisha ongezeko la matukio ya uporaji, sambamba na kuhatarisha usalama wa watumiaji barabara hizo hasa zile za mabasi yaendayo mwendo wa haraka (DART).
“Wananchi baadhi wanalalamika kuwa matukio ya uporaji yameongezeka, na pia usalama umepungua katika maeneo husika,” alisema Makonda.
“Natoa wito kwa wamachinga waondoke barabarani, hatukuweka rami kwa ajili ya wao kufanya biashara, bali zitumiwe na waenda kwa miguu, waendesha vyombo vya moto, tunajua kuwa wanatafuta riziki za familia zao ila wafuate sheria na taratibu za nchi” aliongeza.
Makonda amewataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam ndani ya siku 14 wawe wameshatenga maeneo rasmi ya wafanyabishara ndogondogo ambao hawakupata maeneo.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment