Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Mfalme wa Thailand Bhumibol kuombolezwa mwaka mmoja

Image copyright AP
Image caption Watu wengi waliokuwa nje ya hospitali alimokuwa amelazwa Mfalme Bhumibol walilia kwa huzuni baada ya kifo chake kutangazwa
Raia wa Thailand wameanza kuomboleza kufuatia kifo cha Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye alikuwa nguzo ya uthabiti wa kisiasa nchini humo wakati wa utawala wake uliodumu miaka 70.
Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye ndiye mfalme aliyetawala muda mrefu zaidi duniani, alifariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 88.
Umati mkubwa wa waombolezai walikesha Bangkok wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeusi, na wengi sasa wanarejea katika barabara za mji.

Mwili wa mfalme huyo utapelekwa katika hekalu la Temple baadaye leo.
Maombolezi rasmi yatadumu kwa mwaka mmoja.
Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kwa mfalme mpya, lakini ameomba shughuli yake kurithi madaraka icheleweshwe kidogo.

Maelfu wamejitokeza barabara za Bangkok kusubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo 
 
 
Image copyright AP 
Raia wa Thailand ambao walimchukulia mfalme huyo kuwa nguzo ya uthabiti wamesikitishwa na kifo chake.
Baraza la mawaziri lilitangaza siku ya Ijumaa kuwa siku ya mapumziko.
Bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kwa siku 30 zijazo.
Serikali imewaomba watu wavalie mavazi ya rangi nyeusi na kujiepusha na hafla za "furaha" kipindi hicho.
Tovuti za habari nchini humo zimegeuza rangi za kurasa zake kuwa za rangi nyeusi na nyeupe.
Viongozi mbalimbali duniani wamekuwa wakituma salamu za rambirambi.
Maelfu ya waombolezaji wamefika katika barabara za mji wa Bangkok wakisubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo kutoka hospitali ya Siriraj hadi Kasri Kuu Ijumaa adhuhuri.
Mwanamfalme anayetarajiwa kuwa mrithi wa ufalme ataongoza shughuli za kuosha maiti ya mfalme huyo, tambiko la Kibuddha, Ijumaa jioni, maafisa wa kasri wamesema.

 

Mfalme Bhumibol alichukuliwa kama nguzo ya uthabiti kwenye taifa hilo lililokumbwa na misukosuko ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.
Thailand bado inatawaliwa na jeshi ambalo lilitwaa mamlaka kupitia mapinduzi 2014.
Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kuwa mfalme mpya, amesema tangazo hilo litatolewa baadaye.
Amethibitisha kwamba atatekeleza majukumu yote kama mfalme mtarajiwa, lakini akawataka raia waomboleze kifo cha babake kwanza.

Image copyright AFP
Image caption Mwanamfalme Vajiralongkorn hajafahamika sana na raia wa Thailand
Mwanamfalme Vajiralongkorn, 64 hajafahamika sana na raia wa Thailand na hajapendwa sana na raia kama babake.
Ameishi muda mwingi nje ya nchi, sana Ujerumani.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment