Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Mji wa Kinshasa wanyamaza kimya


KinshasaBiashara zimefungwa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na hakuna magari barabarani kufuatia wito wa upinzani kwa watu wakae ndani katika kushinikiza uchaguzi mkuu nchini ufanyike Novemba na Rais Kabila ajiuzulu.

Mwandishi wa BBC anasema vikosi vya usalama vimeizingira nyumba ya mpinzani mkuu wa rais Kabila, Etienne Tshisekedi, ambye ndiye anayongoza wito wa uchaguzi ufanyike Novemba mwaka huu.

Chama chake kimeonya kuwa rais Kabila atakuwa anatekeleza 'uhaini wa hali ya juu' iwapo uchaguzi utacheleweshwa.
Etienne TshisekediImage copyright Reuters
Image caption Etienne Tshisekedi
Katiba inamzuia Kabila kuwania muhula wa tatu, na upinzani unatuhumu kuwa serikali inataka kuchelewesha uhaguzi huo ili Kabila asalie madarakani.
Chama tawala na kimoja cha upinzani vimependekeza kuchelewesha uchaguzi wa urais hadi Aprili 2018. Kinshasa
KinshasaTume ya uchaguzi inasema inahitaji muda zaidi kuweka sawa orodha ya wapiga kura.
Watu kadhaa wameuawa Kinshasa mwezi uliopita katika maandamano ya kumtaka rais Kabila aondoke madarakani Desemba.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment