Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Mtangazaji wa NBC aliyemuhoji Trump apoteza kazi

 Image result for Billy Bush and trump
Shirika la utangazaji la NBC nchini Marekani limemfuta kazi mtangazaji Billy Bush ambaye amekuwa akiendesha kipindi cha Today.
Mgombea urais wa chama cha Republican alikuwa anahojiwa na Bw Bush miaka kumi iliyopita alipotoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu wanawake.
Ukanda wa mahojiano hayo yaliyofanyika mwaka 2005 ulifichuliwa majuzi na gazeti la Washington Post.
Image result for Billy Bush

Baada ya kufichuliwa kwa ukanda huo, viongozi wengi wakuu wa chama cha Republican walijitenga na Bw Trump ambayo yamezua utata.
Kwenye video hiyo, Bw Bush anasikika akicheka baada ya matamshi ya Bw Trump.
Billy Bush, 45, ambaye ni mpwa wa rais wa zamani George H W Bush, alikuwa awali amesimamishwa kazi baada ya kufichuliwa kwa video hiyo.

Amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Today kwa miezi miwili pekee.
"Ingawa alikuwa mgeni tu katika waandaaji wa kipindi cha Today, amekuwa na NBC kwa muda mrefu. Tunamtakia kila la heri," shirika la NBC limesema kupitia taarifa.
Mke wa Donald Trump, Melania, amemshutumu Bw Bush akisema alimchochea mumewe kusema mambo mabaya kuwahusu wanawake.
Bw Bush mwenyewe aliomba radhi tarehe 7 Oktoba akisema binafsi pia aliaibishwa na tabia yake alipokuwa akifanya mahojiano hayo
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment