Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

South Africa waadhimisha miaka 9 tangu kufariki kwa Lucky Dube

Leo, Oktoba 18, ni miaka 9 tangu mwanamuziki wa nyota wa reggae wa Afrika Kusini, Lucky Dube auawe kwa kupigwa na risasi.
Image result for luck dube
Kwa heshima ya mwanamuziki huyo, waziri wa sanaa na utamaduni, Nathi Mthethwa amelitaka taifa hilo lisherehekee mchango wake kwenye muziki.
“Today we pay tribute to Raggae music icon Lucky Dube who died tragically on this day in 2007. His music touched millions across the globe,” ameandika kwenye Twitter.
 
Moja kati ya nyimbo zilizopendwa sana Together as one.

Oktoba 18, 2007, Lucky Dube aliuawa kwenye kitongoji cha Rosettenville jijini Johannesburg, muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili kati ya saba kwenye nyumba ya mjomba wao.
Polisi wanasema watu waliomuua hawakujua kama nini yeye na walidhani ni Mnaijeria. Watu watano walikamatwa na watatu walipatikana na hatia na kuhukumiwa March 31 2009.
Wawili kati yao walijaribu kutoroka na walikamatwa. Walihukumiwa kifungo cha maisha jela.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment