Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Wavuvi ziwa Victoria watishiwa na mabadiliko ya tabia Nchi

Image result for ziwa victoriaImage caption Mabadiliko ya hali ya hewa hanachangia kuongezeka kwa dhoruba katika Ziwa Victoria 
 
Maisha ya mamia ya maelfu ya wavuvi katika Ziwa Victoria yapo hatarini kutokana na dhoruba kubwa zinazotarajiwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Luven cha Ubelgiji wameonya. 

Takribani watu laki mbili wanategemea ziwa hili kujipatia kipacho chao kama wavuvi au kwa njia nyinginezo.

Ingawa wavuvi wanafahamu fika hatari zinazowakabili wanapokuwa ziwani, hawana njia nyingine mbadala ya uhakika ya kujipatia kipato.

Lakini maelfu ya wavuvi hupoteza maisha yao kila mwaka katika Ziwa Victoria hasa kutokana na mitumbwi na zana nyingine za uvuvi kuwa duni
Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kwamba karibu wavuvi elfu 5 wanapoteza maisha yao kila mwaka katika dhoruba mbaya katika ziwa Viktoria

MarwaImage caption Marwa na wenzake walinusurika baada ya kupigwa na dhoruba wakivua samaki
Wambura Marwa (pichani hapa juu) na wenzake walipaswa kuwa ziwani wakivua siku hii picha hii ilipopigwa, lakini walishindwa kwa sababu, usiku wa kuamkia siku hii walipigwa na dhoruba, mtumbwi wao ukapasuka - waliponea chupuchupu.
"Tulikuwa tumemamiliza siku tatu tukiwa tunavua ziwani, siku ya nne sasa tulipokuwa tunarudi nchi kavu, tulipigwa na dhoruba kubwa sana hadi mtumbwi wetu ukapasuka. Ikabidi tuchukue nguo zetu hizi ndio tukaanza kuuziba mtumbwi mahali ulipopasuka kwa kutumia kisu," anasema Marwa.
"Baada ya kuuziba tukaanza kupiga makasia haraka kurudi nchi kavu na kwa bahati nzuri tulifika kwenye mwaloni salama."
WavuviImage caption Mamia ya wavuvi wamekuwa wakifariki dunia kila mwaka
Wanasayansi kutoka taasisi ya anga ya Marekani, NASA, na chuo kikuu kimoja nchini Ubelgiji, wanaonya kwamba ikiwa hali ya uchafuzi wa hali ya hewa haitadhibitiwa na mabadiliko ya tabia nchi yataendelea, basi mvua katika ziwa zitakuwa nyingi na kubwa maradufu ya zile zinazonyesha nchi kavu.
Hiyo italifanya ziwa Victoria kukabiliwa na dhoruba kubwa na za mara kwa mara.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment