Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Yasemekana sababu haswa ya Scorpion kumtoboa mtu macho ni hii..

Image result for scorpion mtoa macho

Makala hii imeanza kuzunguka katika mitandao mbalimbali ya kijamii leo asubuhi nchini Tanzania, hasa katika jiji la Dar es Salaam, ikielezwa kutoka kwa mkazi wa Buguruni anayesema anakifahamu vyema kisa cha “Scorpion” kumtoaboa macho mkazi wa Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la Said Ally.

Katika habari zilizotolewa na mhanga, alisema kuwa alikuwa akitokea kazini kuelekea nyumbani na alipokuwa akinunua mahitaji yake ya nyumbani eneo la Buguruni, ndipo alivamiwa na mtu huyu anayefahamika kama Scorpion na kumfanyia ukatili huo, huku wananchi wengine wakishuhudia pasi na kumzuia kijana huyo kutoendelea na ukatili wake waziwazi; jambo ambalo wananchi wengi wamekuwa wakihoji kulikoni watu kutoingilia kama jambo hili lilifanywa huku umma ukishuhudia.
Hii hapa chini ndiyo stori mpya inayoeleza kwa upande mwingine sababu za tukio hilo toka kwa mkazi huyo wa Buguruni, ambayo imekuwa ikizunguka katika mtandao wa WhatsApp kuanzia leo asubuhi.
Image result for scorpion mtoa macho
“Inaelekea wanaume wa mkoani na hata hapa Dar es Salaam hawamjui Scorpion. Sisi watu wa Buguruni tunamjua huyo Saidi aliyetobolewa macho, na shughuli zake, na pia tunajua shughuli za Scorpion ndio maana watu hata hawakuhangaika nao kumwokoa Saidi wakati jambo hili linatokea. Watu waliwaacha wamalize mambo yao. Tunaangalia tu watu wanavyo shadadia mambo wasiyoyajua kwa undani wakipiga kelele dunia nzima ikiwa ni pamoja na mkuu wa kaya ya Jiji. Scorpion ni mtu aliyeamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa uwezo huo anao ;kwa maana ya uwezo wa kupambana na mtu yoyote ambae ni mtukutu: napiga kareti kama za kwenye video na physic yake sio ya wanaume hata wawili wa kawaida. He is a man na nyongeza.
Kwa kifupi ni kwamba Buguruni kuna watu watanashati na wana shughuli zao za maana lakini wanamiliki mitandao ya vibaka ambao hupora na kuwaletea mizigo wanayopora. na hiyo ndio wanapopatia hela zao nyingi. Hujawahi kujiuliza Tv, radio, vipochi, simu na vitu vingine kama hivyo vikiibiwa huwa vinaenda wapi? Wale waibaji huenda na kumkabidhi mtu halafu wanapewa hela flani ndogo(ya kula). Yeye huvitakatisha vile vitu kwa kuviuza kupitia legitimate channels (maduka halali) kwa yeye hubaki kuwa mtu legit (safi asiye na hatia).

Scorpion alikua ametangaza kiama kwa vibaka pale Buguruni na alikua anawashughulikia kweli. Hivyo he was posing a danger kwenye biashara za watu. Wakati vibaka wakindelea kushughulikiwa na hali ikionekana imeanza kuwa swari, yani vibaki waliosalia wanahamia kambi nyingine kama Vingunguti, Gongolamboto, n.k ndugu wa kike wa mpiga kareti (rafiki wa Scorpion) akaporwa pochi iliyokua na simu maeneo ya Buguruni Sheli. Hapo ndipo Scorpion akaamua kumsaka muhusika na hakufanikiwa kumtambua. Akaamua kutuma ujumbe kwa mkuu wao ambae ndie mhanga wa macho, kuwa anataka arejeshewe mali iliyoporwa. Kama kawaida ya wapanga misheni mkuu akapiga kimya. Scorpion akaamua kudeal nae, the boss himself ndio akamfuata alipomkuta and the rest of the story baada ya kumfuata face to face mtakua mmeipata kwenye media. Sasa nyie mpeni mamilioni na mitaji bosi wa wahalifu kisa mnamhurumia wakati hamumjui. Ndio maana watu hawakutaka kuingilia kesi wakati jamaa anasulubiwa waziwazi. Sie wa Buguruni tunaelewa. Mtu hakurupuki tu kumtoboa toboa mtu asiyemjua.” – Mwisho.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment