Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

ACT Wazalendo wahofia watoto wa maskini kukosa mikopo

Chama cha ACT Wazalendo kimepinga utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao wanasema ukiachwa bila kupingwa utasababisha watoto wengi wa maskini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo.
act-lll
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii,Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu, amesema chama hicho kimetoa tamko hilo, baada ya takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kuthibitisha kuwa takribani wanafunzi 65,000 wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu, ni wanafunzi 20,000 ndiyo waliopata mikopo.

“Kwanza tulitaka tulitilie mkazo sana suala la watoto maskini kutelekezwa kwenye ugawaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwenye mikoa mingi tuliyotembelea viongozi wa chama wamepinga vikali utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao kama ukiachwa bila kupingwa utawafanya watoto wengi kutoka familia washindwe kujiunga na elimu ya juu. Hali hii imethibitishwa na takwimu iliyokwishatolewa na bodi ya mikopo”,amesema Shaibu.

“Kwenye mikoa mingi iliyotembelewa viongozi wa chama wamepinga vikali utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao kama ukiachwa bila kupingwa utafanya watoto wengi kutoka familia maskini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo,” ameongeza.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment