Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ajira zipo nyingi ila watu wanatatizo la mawasiliano kati ya ubongo na macho – Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka kwa kusema kuwa Tanzania hakuna tatizo la ajira kama baadhi ya watu wanavyofikiria.
rc-makonda-ubungo-15
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipokea heshima kutoka kwa vijana wa skauti wakati ya uzinduzi wa shule ya sekondari ya Urafiki
Akiongea na wazazi pamoja na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa shule ya sekondari ya Urafiki Mtaa wa National Housing Ubungo katika ziara yake ya siku kumi ndani ya mkoa wa Dar es salaam, Makonda alisema kuwa Tanzania hakuna tatizo la ajira kama baadhi ya watu wanavyosema.
“Kama kuna mzazi anadhani Tanzania kuna tatizo la ajira basi huyo mzazi ana tatizo la kuconnect kati ya ubongo na anachokioa katika macho yake,” alisema Makonda. “Tanzania ndiyo nchi pekee isiyo na tatizo la ajira. Tukibadili namna ya kufikiri, Tanzania tuna ajira nyingi sana lakini tukibaki na namna hii tunayoitumia kufikiri hasa kwa kuwaendekeza wanasiasa mchwara tutabaki na tatizo la ajira miaka nenda rudi,”
Aliongeza, “Rais wetu sasa hivi anaendelea kuongelea mpango wa viwanda watu wanambeza kwa sababu wanatatizo la kufikiri, wangekuwa hawana tatizo la kufikiri wangeelewa jinsi viwanda vinavyoongeza ajira. Tumetoka kuangalia viwanda ambavyo Mh DC ametupeleka, tumeona mule ndani vijana wapo wengi sana, na wanampango miaka 2 ijayo wataajiri takribani wafanyakazi 6,000 ndani ya kiwanda kimoja,”
Pia Makonda alisema ndani ya kiwanda hicho kuna vijana 2,000 wa jiji la Dar es salaam ambao wanapata mafunzo katika kiwanda hicho baada ya hapo watapata ajira za kudumu.
Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka diwani wa kata ya Ubungo, Boniface Jacob kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa katika shule ya sekondani Urafiki kwa kujenga madarasa matano.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment