Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

CUF haitauzwa kwa bei poa – Profesa Lipumba

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama hicho hakitauzwa kwa bei poa wala hatoweza kuuziwa mtu yoyote huku akidai chama hicho kimejengwa kwa muda mrefu.
Related image
Akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam, Lipumba alitaka kuwepo kwa maridhiano kati yake na Katibu Mkuu wa hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
“Haiwezi kubadilika kwamba Mwenyekiti wa chama hiki nikiwa hai na Mungu akinijaliwa nikiwa hai mpaka 2019, Maalim waganga watakudanganya sana katika hili lilitakiwe lisifike hapa huna sababu wewe njoo tuzungumze,” alisema. “Pokea simu yangu unajua namba yangu unajua namba yangu tuzungumze, nikupangie kazi tujue namna ya kujenga chama, chama tunahitaji kukijenga Tanzania bara, Zanzibar tulishamaliza,” alisema Lipumba.
“Tunahitaji haki itendeke lakini hatutakubali chama cha CUF kiuzwe, kiuzwe bei poa kwa CHADEMA au kwa Lowassa hilo hatulikubali. Tumekijenga chama hiki kwa muda mrefu na tutaendelea kukijenga kwa hiyo Maalim Seif aache kutafuta huruma ya wananchi kama anahitaji muafaka aje hapa ofisini,” aliongeza.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment