Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ligi kuu Tanzania bara kuendelea wikiendi hii

Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, mzunguko wa 15 unaomaliza duru la kwanza kwa msimu huu, inatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja sita.
soccer-ball-wallpaper-hd-desktop-background-2014-soccer-ball-wallpaper
Kesho Jumapili, African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo Na. 144 wakati Mbao FC itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mchezo Na. 116.
Kwa upande wa Ndanda FC siku ya Jumapili watakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwenye mchezo Na 117 wakati Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo Na. 118.
Kagera Sugar wao Jumapili itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mjini Kagera katika mcpande wake siku hhezo ulipewa Na. 119 ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani kwenye mchezo Na. 120.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu uliopo mkoani Morogoro katika mchezo Na. 113 wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga katika mchezo ulipewa Na. 115.
Source Bongo5
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment