Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Lord Eyez bado yupo Weusi :Joh Makini

Rapper kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amevunja ukimya wa maneno yanayotembea mtaani yanayodai kuwa Lord Eyez amefukuzwa ndani ya kundi hilo.
14032973_680894472063312_21893298_n
Hitmaker huyo wa Perfect Combo amekiambia kipindi cha E News cha East Africa TV kuwa Eyez bado ni mmoja wa wasanii wa kundi hilo.
“Lord hajatengwa na bado ni mmoja wa wanafamilia katika kundi letu la Weusi kuna wimbo wa Lord tulikuwa studio tukiuandaa juzi. Watu wanaongea mengi kuhusu ukaribu wetu na Lord kwa sasa ila si mbaya wakituzungumzia kwa kuwa ni sehemu ya maisha yetu,” amesema Joh.
Kundi la Weusi linaundwa na wasanii watano akiwemo Joh makini, Nick wa Pili, G-Nako, Bonta na Lord Eyez.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment