Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Maelfu wapinga ushindi wa Trump

Maelfu ya Wamarekani wameandamana kwenye mitaa ya miji mbalimbali nchini humo kupinga ushindi wa Donald Trump.
161109213121-09-trump-protest-1109-restricted-exlarge-169
Walisikika wakisema kauli za kumpinga Trump na kukusanyika nje ya ikulu ya White House.
“Not my President, not today,” wengi walisikika wakisema.
Katika majiji kuanzia Boston hadi Los Angeles, maelfu ya waandamanaji walikusanyika usiku wwa Jumatano kupinga kuchaguliwa kuwa rais bilionea huyo ambaye kampeni yake iligubikwa na kashfa kibao.
Zaidi ya watu 5,000 waliandanama jijini New York. Mamia walionekana nje ya jengo linalomilikiwa na rais huyo mteule, Trump Tower jijini humo. Wengi walioandamana ni wahamiaji nchini humo ambao wana wasiwasi kuwa sera za Trump zitayafanya maisha yao kuwa magumu.
Maandamano mengi yamefanyika kwenye majiji yenye wafuasi wengi wa chama cha Democratic yakiwemo Atlanta; Austin, Texas; Boston; Chicago; Denver; Philadelphia; Portland, Oregon; San Francisco, Seattle na Washington.
Hizi ni picha zaidi:
161109221457-11-trump-protest-1109-exlarge-169
161109211059-03-trump-protest-1109-exlarge-169
161109211102-04-trump-protest-1109-exlarge-169
161109211105-05-trump-protest-1109-restricted-exlarge-169
161109211107-06-trump-protest-1109-exlarge-169
161109211108-07-trump-protest-1109-restricted-exlarge-169
161109211110-02-trump-protest-1109-exlarge-169
161109213123-08-trump-portest-1109-exlarge-169
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment