Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Mamadou Sakho kuondoka Liverpool huenda akajiunga na Olympique Marseille


Klabu ya Olympique Marseille kutoka nchini Ufaransa, imeonyesha nia ya kumsajili beki wa kati wa majogoo wa jiji (Liverpool) Mamadou Sakho.
mamadou-sakho-559x520
Sakho ameshafunguliwa mlango wa kuondoka na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, kwa kuambiwa anaweza kuondoka wakati wa majira ya baridi (Mwezi Januari).
Olympique Marseille wanajiandaa kuwasilisha ofa ya usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 26.
Mchezaji huyo alisajiliwa na Liverpool mwaka 2013 akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain.

Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment