Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Mfalme mteule wa Thailand kuthibitishwa Desemba mosi

Mwana mfalme VajiralongkornMwana mfalme Vajiralongkorn
BBC imetaarifiwa kwamba mfalme mteule mtarajiwa wa Thailand Vajiralongkorn atathibitishwa rasmi kama mfalme ajaye mnamo Desemba mosi
.
Mwana wa mfalme huyo ambaye pia ni mfalme mtarajiwa alitarajiwa kupakwa mafuta na kutawazwa katika kipindi ama baada ya maziko ya babake , mfalme King Bhumibol Adulyadej, aliyefariki wiki tatu zilizopita, kutokana na yeye mwenyewe kuomba muda wa kumuomboleza babake.
Vajiralongkorn ana mtoto mmoja wa kiume aliyempata na mke wake wa zamani SrirasmiVajiralongkorn ana mtoto mmoja wa kiume aliyempata na mke wake wa zamani Srirasmi
Mpaka sasa haijafahamika wazi, ni uhusiano wa namna gani mfalme huyo mtarajiwa atakuwa nao baina yake na vikosi vya jeshi la serikali ambavyo hivi karibuni vilikuwa vinaiongoza Thailand, ama ni namna gani atapokelewa na raia wake.
Vajiralongkorn katika mbio za baiskeli mwaka 2015Vajiralongkorn katika mbio za baiskeli mwaka 2015
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment