Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ricardo Kaka atamani kurejea Brazil kuichezea timu hii

Mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid, Ricardo Kaka, ametangaza mustakabali wa kucheza soka lake akiwa nchini Marekani.
maxresdefault
Kaka ametangaza mustakabali wake wa soka nchini Marekani alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Fox Sports, ambapo hata hivyo alisita kueleza kwa kina ni wapi alipolenga kucheza soka lake kwa mwaka 2018.
“Msimu ujao utakua wa mwisho kucheza Orlando City, na bado sijaelewa nitaelekea wapi, lakini nitapenda kurejea nyumbani Brazil na klabu ambayo nitataka inisajili ni Sao Paulo.
“Nitajitahidi kadri niwezavyo ili niweze kuondoka Orlando City kwa heshima msimu ujao, nitapambana kwa kusaidiana na wenzangu ili tufanikishe jambo kubwa ambalo litakua na kumbukumbu kwangu na kwa klabu kwa ujumla.
“Kwa wakati wote tangu mwaka 2014, nimekua na furaha nikiwa hapa, na ninaamini suala hilo lilichangia kiwango changu kuonekana kwa kushirikiana na wengine.” Alisema Kaka

Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment