Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ronaldo kusaini mkataba mpya Real Madrid hadi 2021Klabu ya Real Madrid imetangaza rasmi kuwa nyota wao Cristiano Ronaldo, November 7/11/2016 jumatatu atasaini kandarasi mpya itakayomfanya aitumikie timu hiyo mpaka mwaka 2021 (atakuwa na umri wa miaka 36).
3a1c5ea500000578-3910084-image-a-16_1478428633629
Kazi kubwa iliyofanywa na rais Florentino Perez, ambaye kwa kiasi kikubwa alichukua jukumu la kuzungumza na nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno.
“Ronaldo atasaini mkataba mpya baadae hii leo, na kisha atazungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Santiago Bernabeu stadium kuanzia saa saba na nusu mchana” imeeleza taarifa iliyotolewa na Real Madrid.
“Mshambuliaji huyo kutoka nchini Ureno atasaini mkataba ambao utamuweka hapa hadi Juni 30-2021, atakua sambamba na rais wa klabu Florentino Perez, katika mkutano na waandishi wa habari.” Imeongeza taarifa hiyo
Ronaldo anakua mchezaji wa pili kukubali kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia Real Madrid, akitanguliwa na Gareth Bale ambaye alifanya hivyo juma lililopita.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, alijiunga na Real Madrid akitokea Manchester United kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 80 ambayo iliweka rekodi ya dunia kwa mwaka 2009.
Mpaka sasa ameshaifungia klabu hiyo mabao 350, sambamba na kutwaa ubingwa wa Ulaya mara mbili, ubingwa wa ligi ya Hispania mara mbili, ubingwa wa kombe la Mfalme mara mbili, Supercopa mara mbili, UEFA Super Cup na klabu bingwa duniani (FIFA Club World Cup) mara moja.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment