Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

aliyetaka kumuua Donald Trump ahukumiwa mwaka mmoja jela

Kijana aliyetaka kumuua Rais mteule wa Marekani, Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela.

Mtuhumiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Michael Sandfgord mwenye umri wa miaka 20 alikamatwa na polisi baada ya kutaka kumpokonya bunduki polisi ili kumuua Trump kwenye kampeni huko Las Vegas.
Sandfgord ambaye ni raia wa Uingereza anadaiwa kuwa alikuwa akiishi nchini Marekani bila ya kuwa na kibali baada ya kutoroka nchini kwao. Hata hivyo imedaiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Sandfgord akaachiliwa baada ya kutumikia miezi minne ya kifungo chake.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment