Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Awamu ya tano: Vilio vya mijini ni furaha vijijini

Ukipatwa na kiu ya maji unahitajika kupata kimiminika hicho ili kuweza kukata kiu hiyo lakini ukikosa utahaha mpaka utahisi roho inataka kukutoka.
magu1-1
Ni muda mrefu wakulima na wakazi wa vijijini wamekuwa na kiu ya maji kuweza kukata kiu waliokuwa nayo lakini waliyakosa huku nyuso zao zikiwa na huzuni kubwa. Ukiwatazama midomoni kuna kitu wanataka kusema lakini walikuwa wanashindwa kutokana na kitu kizito kilichozuia midomo yao isiweze kutamka chochote zaidi ya macho yao kutoa machozi muda wote.
Baada ya kilio cha muda mrefu kwa watu hao bila ya kujua hatima yao, ghafla inakuwa kama vile ‘mtu aliyehukumiwa kifo lakini kabla ya siku yake ya hukumu anataarifiwa kuwa yupo huruni’.
Pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweza kuwafuta machozi wakulima wetu wadogo wadogo ambao walikuwa tayari wameshakata tamaa kutokana naa kilimo chao huku kila mmoja akitamani kuja mjini kutafuta njia mbadala ya kuweza kufanikiwa kimaisha – hakika kwa hili la sasa watu wa mijini ndio tutakaokimbilia vijijini kuanza kutafuta mashamba na kuanza kulima.
Wakati mijini watu wakilia maisha magumu, furaha imetawala vijijini ikiwemo kwa wakulima wa mazao ya korosho kwenye mikoa ya kusini baada ya mwaka huu kuuza mazao yao hayo kwa zaidi ya shilingi 3500 kwa kilo kitu ambacho hakijawahi kutokea wakati hapo awali walikuwa wakiuza kwa kiasi kisichozidi 1500 kwa kilo. Wakati huo huo baadhi ya wakazi vijiji vingine wameanza kusogezewa huduma muhimu za kijamii karibu ambazo hawajawahi kuziona kwenye maendeo yao tangu wazaliwe.
Ni ukweli usiofichika kuwa watu wengi wa mijini tumekuwa tukiishi maisha ya kujipatia fedha kwa njia za ujanja ujanja ndio maana kipindi hiki cha uongozi wa Rais Magufuli tumekuwa tunalalamika maisha magumu wakati kama mshahara uliokuwa ukiupata ndio ule ule unaopokea sasa – hapo tunaona kuwa kuna vitu vingine vilivyojificha tulikuwa tunafanya.
Je kwa baadhi ya viongozi serikali walikuwa wakijilundikia mali nyingi pamoja na fedha za umma, kulikuwa na umuhimu gani wa kufanya hivyo wakati kuna kijiji hakina hata zahanati moja wala huduma ya maji wamekuwa wakitembea umbali mrefu zaidi kufata huduma hiyo kwa miaka mingi zaidi?
Hiko ndicho kilichokuwemo hapo mwanzo lakini kwa kasi ya uongozi wa Rais Magufuli kwa asilimia kubwa amepunguza hali hiyo huku operasheni ya “Kutumbua Majipu” ikiwaamsha usingizini viongozi wengine walilala kuanza kuchapa kazi.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment