Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Hali ya maisha inapokuwa ngumu basi ujue kuna utimilifu na ukamilifu mbele yako – Ray C

Msanii mkongwe wa muziki Ray C ameamua kuyapotezea yale yanayozungumzwa katika mitandao ya kijamii baada ya jana mtandao wa Global Publisher kuandika taarifa inayodai kuwa muimbaji huyo wa wimbo ‘Milele’ anajiuza.

Image result for ray c

Kwa mujibu wa taarifa za mtandao huo zinadai kuwa haikuwa kazi rahisi fuatilia mkasa huo mpaka walipowatumia Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya mtandao huo.
Muimbaji huyo ambaye ameweza kupambana kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya, ameona siyo vyema kukaa kimya na kuamua kuzungumza kuhusu issue inayozungumzwa.
Kupitia mtandao wa Instagram, Ray C ameandika:
Maisha ni Safari ndefu,unapoona hali ya maisha inakuwa ngumu basi ujue kuna utimilifu na ukamilifu mbele yako, usikatishwe tamaa na maneno ya binadamu wenzio ambao wana miguu miwili kama wewe na wameumbwa na yuleyule aliekuumba wewe na ambao nao hawajui hatma ya maisha yao kama vilevile usivyojua hatma yako,kesho yako usivyoijua basi ujue hakuna binadamu anaeifahamu kesho yake itakuwaje!kumbuka mtabiri na mwongozaji wa maisha yako ni mmoja tu aliekuumba wewe na ndie peke yake wa kumtegemea katika kila jambo maishani mwako,dunia na watu wake na vitu vyake na mambo yake yataendelea kuwepo tu muhimu ni wewe kujua unasimama upande upi salama katika kufanikisha kile unachokidhamiria kwenye maisha yako, muhimu ni kuwa na imani matumaini na ujasiri wa kufanikisha jambo lako,funga skio la nafsi haribifu za utabiri wa dunia za munguwatu na sikiliza nafsi yako ndani yako iliyo ya ukweli na nia kufikisha malengo yako maishani mwako, jiamini jikubali sema kwa nguvu ya Mungu ntafanikisha nitakalo maishani! ongea na Mungu wako katika kila jambo mshirikishe yeye Kwani kuna nguvu ya Mungu inayotembea na sisi wakati wote ni kuamini tu kwamba mbele yake yeye muumba mwenye dunia yake hakuna linaloshindikana chini ya jua!kuwa na imani na yeye tu!hakuna mwingine mwenye upendo wa kweli kama Mungu. 
Muimbaji huyo kwa sasa amekuwa akijichimbia katika studio za Wanene kuandaa kazi zake mpya ambazo bado hajazizungumzia.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment