Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Huku CBE kule TIA mabingwa mashindano Green City Inter-College Tournament 2016


Mashindano ya Green City Inter-College Tournament yanaliyoshirikisha  vyuo vikuu na vya kati jijini Mbeya  , yamemalizika jijini hapa baada ya kuzinduliwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 26 Novemba 2016.CBE ndio Mabingwa wa Mashindano ya Vyuo Vikuu Mbeya "GREEN CITY INTER-COLLEGE TOURNAMENT" baada ya kuwabwaga Timu ya Chuo cha SAUT kwa mikwaju za penalti.
Kwa upande wa mchezo wa Netball Timu ya Chuo cha T.I.A waliochomoza na ushindi wa magoli 18 dhidi ya magoli 16 ya Timu ya Netball ya Chuo cha TUMAINI-MAKUMIRA, na kuibuka mabingwa.
 Vyuo vilivyoshiriki  katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na kuendeshwa na  kituo cha redio cha Dream FM cha jijini Mbeya, ni pamoja na  Chuo cha Uhasibu (TIA), Theofilo Kisanji (TEKU), St. Augustine (SAUT),  na Mzumbe , Vyuo  vingine vinavyoshiriki mashindano hayo ni  Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST),  Tumaini Makumira, Chuo cha Kilimo Uyole, na VETA, ambapo kila chuo kilishiriki katika michezo ya mpira wa miguu na mpira wa pete.  


Mashindano hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza jijini hapa na yamekuwa yakiendesha kwa njia  ya mtoano tangu siku ya ufunguzi November  26, yamekuwa na msisimko mkubwa kwa wanavyuo wa vyuo vyote shiriki na wadau mbalimbali wa michezo jijini hapa.
 Akizungumza na waandishi wa  habari, meneja mkuu wa kituo cha redio Dream FM bwana Grayson Kayombo , amesema kuwa lengo kubwa la kuandaa mashindano hayo ni kuwapa fursa wanafunzi wa elimu ya juu na kati kukutana kwa pamoja na kuonesha vipaji vyao, hasa kwa kuzingatia kwamba kwa sasa michezo imekuwa  miongoni mwa sekta zinazotoa fursa za ajira kwa vijana katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Bwana Kayombo aliongeza kuwa mashindano hayo yamelenga kuwajengea wanafuzi na vijana kwa ujumla utamaduni wa kushiriki katika michezo na mazoezi ya viungo kwani ni njia madhubuti ya kuwajengea afya njema hivyo kuweza kushiriki ipasavyo katika masomo na shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa.
 Bwana Kayombo aliendelea kwa kusema kuwa  kwa kushiriki katika michezo, vijana hujenga tabia ya umoja miongoni mwao, ujasiri wa kufikia malengo yao, na kuepuka kushiriki katika matukio na tabia zisizo na staha mbele ya jamii zinazowazunguka.
 Aidha meneja huyo wa kituo cha redio Dream FM aliwashukuru wadau mbalimbali hasa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kilimanjaro Premium Lager, na Ally Rich Sanaa (ARTS) Ltd  kwa mchango wao mkubwa  katika kufanikisha mashindano hayo.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanavyuo, rais wa serikali ya wanachuo wa Chuo cha Uhasibu (TIA), bwana Ahmad Lupatu amesema kwamba wanafunzi na uongozi  wa vyou vyote vinavyoshiriki katika mashindano hayo hawana namna ya kuweza kueleza shukrani na hisia  zao za kipekee kwa redio Dream FM kwa kuandaa mashindano hayo na kutoa seti ya jezi za kisasa na mipira kwa timu zote kumi na sita zinazoshiriki katika mashindano hayo.
 Kiongozi huyo kwa niaba ya wanavyuo  alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanavyuo na kuongeza  kwamba Green City Inter- College ndiyo habari ya mjini kwa sasa vyouni jijini humo.
Kwa upande wake mkuu wa Chou cha VETA mkoa wa Mbeya  bwana  Lameck P. Kihinga, baada ya kupokea vifaa vya michezo kutoka kwa  meneja wa redio Dream FM bwana Grayson Kayombo, alisema kuwa kituo hicho cha redio kimefanya jambo la kipekee  na linalopaswa kuigwa  na kwamba kituo hicho kinadhihirisha kwa matendo kwamba kimekusudia kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao, na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo za redio Dream FM.
Mashindano ya Green City Inter-College Tournament 2016 yalikuwa yakifanyika katika viwanja vya vyuo vya TEKU na TIA  kwa juma.
 Aidha baada ya michezo ya fainali na CBE kuondoka na ushindi kwa upande wa wanaume na TIA kwa upande wa wanawake, kulifuatwa na tamasha kubwa la kufunga mashindano hayo, lililopewa jiwa la Green City Inter-College Back to Campus Bash lilofanyika katika ukumbi wa Club K-MO uliopo Soweto jijini Mbeya, ambapo pamoja na burudani  kutoka kwa wasanii mbalimbali, wanachuo walipata fursa ya kuonesha vipaji vyao kama vile vya kuimba, kucheza, kuigiza, kupiga vyombo vya muziki, na vingine vingi.
Washindi wa kwanza, wa pili, na wa tatu wa michezo yote walipata zawadi za fedha taslimu kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo redio Dream FM.


Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment