Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Kanye West aeleza kwanini alikutana na Donald Trump

Kanye West ameendelea kutengeneza vichwa vya habari. Awamu hii ni baada ya kukutana na Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump jijini New York, Marekani.

Jamii ya watu weusi imemkosoa vikali kwa kitendo chake hicho. Hata hivyo rapper huyo amelazimika kueleza kupitia Twitter kwanini amekutana na bilionea huyo. Amedai alitaka kuzungumza naye masuala mbalimbali ikiwemo unyanyasaji, kusaidia wwalimu, kuboresha mitaala ya kufundishia na ukatili jijini Chicago.

“I wanted to meet with Trump today to discuss multicultural issues,” alitweet. “These issues included bullying, supporting teachers, modernizing curriculums, and violence in Chicago. I feel it is important to have a direct line of communication with our future President if we truly want change.”

Wakati huo huo kukutana na Trump kumemfanya abadilishe wazo lake la kugombea Urais mwaka 2020. Rapper huyo ametweet #2024.
Hizo ni tweets zake za kwanza tangu alipolazwa hospitali.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment