Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ombi la Mawakili wa Lema kwenye kesi ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alikamatwa November 2 2016 akiwa Dodoma hadi leo anashikiliwa katika gereza kuu la Kisongo Arusha kutokana na kusudio la Mkurugenzi wa mashtaka kupinga uamuzi wa hakimu mkazi wa Arusha, Desdery Kamugisha aliyempa dhamana katika kesi ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. 

Leo December 8 2016 Mawakili wa Lema wamewasilisha ombi  mahakama kuu kanda ya Arusha kuomba kuongezewa muda wa kuleta notisi ya rufaa ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema
Wakili wa mbunge Lema Shedrack Mfinanga amesema kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo na jaji Opio, lakini upande wa Jamhuri uliomba kuandaa kiapo kinzani na mahakama imepanga kusikiliza kesi hiyo December 14 2016.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment