
Kuna
matukio ambayo yamezoeleka kufanywa na binadamu lakini inapokuja suala
la wanyama kuwekewa sheria ambazo zimekuwa zikitumiwa na binadamu, jambo
hilo huleta maswali mengi kama hii ya nchi ya Iran iliyoamua kuweka
sheria kwa Ngamia kuwa na Plate Numbers ili kupunguza matukio ya ajali.
Mpaka
sasa inaelezwa kuwa tayari wanyama takribani laki moja nchini Iran
wamepewa namba za usajili huku wengine 35,000 wakipangwa kusajiliwa
kabla ya mwaka huu kumalizika, na sababu kubwa ya kufanya hivyo imetajwa
kuwa kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani.


Maafisa
wa usalama nchini Iran wameanza kutekeleza sheria hiyo kwa majaribio
kwenye miji ya Sistan na Baluchestan ambayo iko mpakani mwa Afghanistan
na Pakistan ambako kumekuwa na matukio ya uharibifu wa mali na ajali za
mara kwa mara.
Mohammad-Sharif Khaleqinia, ambaye ni katibu mkuu wa Central Task Force ameuambia mtandao wa IRNA: “Tunatarajia
kutoa namba za usajili kwa wanyama aina ya Ngamia wapatao 35,000 mpaka
kufikia mwisho wa mwaka huu, lengo letu ni kutaka kutambua mmiliki
halali wa wanyama hawa”.
Kwa mujibu wa IFP News,
lengo lingine la serikali ya Iran ni kuwafanya wananchi watimize
majukumu yao ya kutunza wanyama wanaowafuga ikiwa ni pamoja na kupunguza
au kuondoa kabisa wanyama wanaozurula mitaani na kusababisha usumbufu.
0 comments:
Post a Comment