Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Simba yaongeza nguvu kikosini wamleta mshambuliaji mpya kwenye kikosi chake

Klabu ya soka ya Simba SC inaendelea na usajili wa kuboresha kikosi chao kwa ajili ya raundi ya pili ya ligi kuu msimu huu.

Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva akiwa na Pastory Athanas
Katika kuboresha kikosi hicho, timu hiyo imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa timu ya Stand United ya Shinyanga, Pastory Athanas.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba huo Jumanne hii mbele ya mwenyekiti wa Simba, Evans Aveva. Kwa sasa timu hiyo itakuwa na washambuliaji wasiopungua wanne, akiwemo Laudit Mavugo, Ibrahim Ajibu, Mohammed Ibrahim, Blagnon na wengine.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment