Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Taarifa mbaya kwa mashabiki wa Everton kutoka kwa BolasieMchezaji wa klabu ya Everton Yannick Bolasie, atafanyiwa upasuaji wa goti baada ya uchunguzi kubaini kwamba alipata jeraha baya kwenye kano za goti walipokuwa wakikabiliana na Manchester United siku ya Jumapili.
3b09404d00000578-4002906-image-a-1_1480966621008
Bolasie ambaye ni raia wa DR Congo ameshiriki mechi zote msimu huu kwenye klabu ya Everton.
Bolasie, 27, alipata jereha katika mguu wake wa kulia dakika ya 68 ya mchezo siku ya Jumapili ambao mchezo huo walipotoka sare ya 1-1 katika uwanja wa Goodison Park.
3b08517400000578-4002906-image-a-13_1480967086102
Bolasie, alichezea klabu ya Crystal Palace kwa misimu minne baada ya kutoka Bristol City mwaka 2012 kabla ya kuhamia Everton.
Nyota huyo hatashiriki michuano ya Kombela Taifa Bingwa Afrika nchini Gabon mwezi ujao.
Kabla ya jeraha la Bolasie, meneja wa Everton Ronald Koeman, alikuwa amezungumzia suala la kusajili mshambuliaji wa Manchester United Memphis Depay, 22, kwa mkopo ifikapo mwezi Januari.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment