Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Timu ya Chapecoense yatunukiwa kombe la Copa Sudamericana

Klabu ya Chapecoense kutoka Nchini Brazil, ambayo iliwapoteza wachezaji 19 pamoja na wahudumu kwenye ajali ya ndege walipokuwa wakielekea kucheza fainali ya Copa Sudamericana, imetunukiwa kombe hilo.
_92843236_brazil1_getty
Mashabiki na jamaa wakitoa heshima zao kwa wachezaji waliofariki katika ajali hiyo ya ndege
Uamuzi huo umechukuliwa na shirikisho la soka la Amerika Kusini, Conmebol kufuatia ombi la wapinzani wa klabu hiyo.
Watu 71, wakiwemo wachezaji 19 na wahudumu wa klabu hiyo, walifariki Jumatatu wakielekea Colombia kwa mechi ya mkondo wa kwanza ya fainali ya kombe hilo.
_92815129_mediaitem92815128
Wapinzani wa klabu hiyo kutoka Atletico Nacional, ambao waliomba Chapecoense wapewe kombe hilo, wametunukiwa tuzo ya Uchezaji Haki ili kutambua “moyo wao wa amani, kuelewa na kucheza haki”.
Chapecoense pia watapewa jumla ya $2m (£1.57m) ambazo hukabidhiwa mshindi.
Atletico Nacional nao watapewa $1m (£787,000).
Makamu wa rais wa Chapecoense Ivan Tozzo amesifu uamuzi huo na kuutaja kama “haki”, akihutubia wanahabari Jumatatu.
“Tuna uhakika ‘Chape’ wangekuwa mabingwa. Ni heshima kubwa.”
Wachezaji watatu wa Chapecoense ni miongoni mwa watu sita walionusurika ajali hiyo.
Brazil watacheza dhidi ya Colombia mechi ya kirafiki mwishoni mwa Januari kuchangisha pesa za kusaidia waathiriwa wa ajali hiyo ya ndege.
Source: BBC
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment