Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Yanga yafanya maamuzi magumu kwa Mbuyu Twite

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Yanga wamethibitisha rasmi kuachana na mchezaji wao Mbuyu Twite na nafasi yake kuchukuliwa na Justine Zulu wa Zambia.
img_0398
Baraka Deud Edith amethibitisha kuachwa kwa Twite wakati alipokuwa akiongea na Radio EFM katika kipindi cha Sports HQ.

Aidha sheria za TFF kwa timu za ligi kuu zinasema kuwa kila timu ya ligi kuu inapaswa kusajili wachezaji wasiozidi saba, hivyo Yanga walikuwa na wachezaji nane.

Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwezi huu wa Disemba huku akiwa na nafasi ya kufanya mazungumzo na timu yoyote inayo muhitaji kutokana na kanuni za sheria za mchezo wa soka.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment