Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Al-Shabab lawaua wapelelezi kutoka Kenya na Marekani

Wapiganaji wa kundi la Al-ShababHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWapiganaji wa kundi la Al-Shabab
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia wamewaua watu 3 inaowatuhumu kwa kulipelelezea shirika la ujasusi nchini Marekani CIA pamoja na vitengo vyengine kulingana na tovuti ya Somali Memo inayounga mkono kundi hilo.
Watatu hao waliuawa mbele ya kundi kubwa la watu kusini magharibi mwa mji wa Yaq-Barawe.
Abdullahi Damey Mohamud Nur mwenye umri wa miaka 36 alipatikana na hatia ya kulichunguzia kundi la CIA kutoka Marekani ambapo alikuwa akipokea mshahara wa dola 200 kila mwezi, kulingana na mtandao huo.
Jaji wa al-Shabab alisema kuwa Mohammed alikiri kuwasaidia Marekani kwa kutekeleza mashambulio kwa kutumia ndege zisizo na rubani.
Jaji huyo pia alisema kuwa Mohamed Iman Hassan mwenye umri wa miaka 42 aliuwawa kwa kupelelezea Kenya na alikuwa akipata dola 150 kama mshahara.
Mohamed Sharrif Ali mwenye umri wa miaka 21,alituhumiwa kwa kuisaidia mamlaka ya Jubbaland kukusanya habari kuhusu kundi hilo.
SOURCE BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment