Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Je Trump atamteua Mkwe wake, kama mshauri wake?

Jared Kushner akiwa na mkewe binti wa Trump

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJared Kushner na mke wake
Rais Mtarajiwa wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kumteua mkwe wake Jared Kushner, kama Mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.
Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.
Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.
Uteuzi huo unatarajiwa kwa kiasi kikubwa, na hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.
Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.
Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment