Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Marehemu aonekana kwenye picha za harusi

Catherine Flower, Shaun CarterHaki miliki ya pichaJELLY PENGUIN GRAPHICS/ CATHERINE FLOWER
Image captionCatherine anaonekana akiwa na mamake na babake wa kambo na kunayo picha ambayo haijakolea sana na nduguye anayeoneakana kuweka mikono yake kwenye bega la Catherine.
Bi harusi, ambaye kakake alifariki wiki chache kabla yake kufunga ndoa, amechukua hatua isiyo ya kawaida kwa kuongeza picha za kakake huyo katika zake za harusi Uingereza.
Kakake Catherine Carter, Shaun Carter, alifariki kwenye ajali Mei lakini alipofunga pingu za maisha Julai aliomba usaidizi kutoka kwa mtaalamu wa picha kuongeza picha za Shaun kwenye picha za harusi.
Katika picha moja, Catherine anaonekana akiwa na mamake na babake wa kambo na kunayo picha ambayo haijakolea sana na nduguye anayeoneakana kuweka mikono yake kwenye bega la Catherine.
Alisema: "Ni mwujiza kumuona kwenye picha zangu za harusi, sikuweza kujizuia kutokwa na machozi."
Seeing him in the pictures was a miracle, I couldn't stop crying."

'Heartbreaking'

Shaun, 29, alifariki katika ajali eneo la mjengo Cirencester, eneo la Gloucestershire, mwishoni mwa mwezi Mei.
Catherine, aliolewa na John Flower katika kanisa la St Paul's, Chippenham mwezi Julai.
Catherine Flower na Shaun CarterHaki miliki ya pichaJELLY PENGUIN GRAPHICS/ CATHERINE FLOWER
Image captionPicha hizo zimependwa zaidi ya mara 2,000
Rachel, wa kampuni ya Jelly Penguin Graphics, ambayo iliunda picha hizo, amesema ombi la Catherine lilimgusa sana.
Tangu picha hizo zipakiwe kwenye Facebook, zimependwa na zaidi ya watu 2,000 na mamia ya watu wametolea maoni.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment