Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Marekani kuanza kuitoza Mexico kodi ya bidhaa zake ili kufidia ujenzi wa Ukuta

Rais Pena Nieto na Rais TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Pena Nieto na Rais Trump
Ikulu ya Marekani imesema Rais wa nchi hiyo Donald Trump anaweza kutoza asilimia 20 ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka Mexico kuweza kusaidia mpango wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili kuzuia kuingia kwa Wahamiaji haramu na madawa ya kulevya.
Mexico imesisitiza kuwa haitolipia gharama za ujenzi wa ukuta huo na kwamba pendekezo hilo jipya lililotolewa litasababisha kuzidisha ufa wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kusababisha Rais Enrique Pena Nieto kufuta ziara yake ya kukutana na Rais Trump wiki ijayo mjini Washington.
Uamuzi wa Rais Pena Nieto umeungwa mkono nchini mwake, akiwemo pia mtangulizi wake Vicente Fox.
Bwana Fox amesema ana uhakika Mexico italipiza kisasi kwa kutoza kodi bidhaa zitokazo Marekani, iwapo mipango hiyo ya Rais Trump itatimizwa.
Katika Hatua nyingine Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Trump.
Mpaka wa Mexico na MarekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTayari kuna ukuta katika sehemu za mpaka wa Marekani na Mexico ambao una umbali maili 2,000 (3,200km)
Katika ziara yake nchini Marekani tayari amekutana na wanachama wa Republican mjini Philadelphia ambapo amesema Uingereza na Marekani hazipaswi kurudi katika kile alichokiita sera za uvamizi zilizoshindwa, walizokuwa wakizitumia awali.
Hata hivyo amesema nchi hizo mbili bado zina jukumu la kuongoza dunia.
SOURCE BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment