Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Moshi Mchafu Beijing wabuniwa kikosi cha kupambana

Kikosi kipya cha kushughulikia masuala ya mazingira kinatarajiwa kupunguza viwango vya moshi mchafu unaotaka kweny mji wa Beijing nchini China.
Polisi hao watakuwa wakitafuta vyanzo vya moshi huo yakiwemo maeneo ya nje ya kuchomea nyama na barabara zenye vumbi, kwa mujibu wa meya wa mji huo Cai Oi.
Meya pia ameahidi kupunguza matumizi ya makaa ya mawe kwa asilimia 30.
Wakaazi wengi wa mji wa Beijing wamelazimika kubaki manyumbani mwao kwa siku kadha ili kuzuia kupumua moshi huo mchafu.
Watu wamekuwa wakitoa wito kwa serikali kufanya jitihada zaidi kupunguza moshi huo, ikiwemo kupunguza viwanda vinavyotegemea nishati ya mkaa wa mawe.
Watu wamekuwa wakijifunika ili kuzuia kupumua moshi huo mchafuImage copyrightAP
Image captionWatu wamekuwa wakijifunika ili kuzuia kupumua moshi huo mchafu

SOURCE BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment