Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ni Ronaldo tena, ashinda tuzo za FIFA

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA

RonaldoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRonaldo ametajwa kuwa mcheza kandanda bora wa dunia

Ronaldo, 31, amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d'Or mwezi Disemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa na timu ya taifa ya Ureno.
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri ametajwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, huku Silvia Neid, meneja wa zamani wa Ujerumani, akishinda kwa upande wa wanawake.
SOURCE BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment