Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Rais mpya Ghana aapishwa, viongozi waliohudhuria sherehe hiyo kujadiliana namna ya kumchomoa Rais wa Gambia aliegomea madarakani

Rais mpya wa Ghana ambaye aliwahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu hapo zamani, Nana Akufo-Addo, ameapishwa rasmi leo kuwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo, katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Independence Square Jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.

Katika hotuba yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais aliyemaliza muda wake madarakani, John Dramani Mahama, kwa namna alivyokiri kushindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Viongozi zaidi ya 14 kutoka nchi za Afrika walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais huyo mpya, Nana Akufo Addo.
Rais Akufo Addo, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani.

Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment