Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Shirika la Marekani kumshtaki Trump kuhusu malipo

Trump Tower New York. 21 Jan 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump humiliki hoteli na majumba mengi
Shirika moja la kisheria nchini Marekani limetangaza kwamba litawasilisha kesi dhidi ya Rais Donald Trump.
Shirika hilo linamtuhumu kiongozi huyo kwa kikiuka marufuku iliyowekwa kwenye katiba dhidi ya kupokea malipo kutoka kwa serikali za nchi za nje.
Kundi la mawakili na watafiti linasema Bw Trump amekuwa akipokea malipo kutoka kwa serikali za nje kupitia wageni kwenye hoteli zake na majumba yake ya kukodisha.
Wanasema kuna kifungu kwenye sheria ya nchi hiyo ambacho kinaharamisha malipo kama hayo.
Mwanawe Donald Trump, Eric, ametaja hatua hiyo kama "usumbufu tu kwa nia ya kufaidi kisiasa".
Eric Trump, ambaye ni makamu rais mtendaji wa shirika la Trump Organization ambalo linamiliki na kusimamia biashara za rais huyo, amesema kampuni hiyo imechukua hatua kubwa kufuata sheria kuzuia kesi, kwa mujibu wa New York Times.
Amesema kampuni hiyo imeahidi kutoa faida kutoka kwa hoteli zake ambazo zimetokana na wageni kutoka serikali za nje na kuziwasilisha kwa Hazina Kuu ya Marekani.
'Tumelazimishwa kuchukua hatua'
Shirika hilo la Citizens for Responsibility and Ethics in Washington (Crew) limesema litawasilisha kesi katika mahakama ya Manhattan, New York Jumatatu asubuhi.
"Hatukutaka kufika hapa," mkurugenzi mkuu mtendaji Noah Bookbinder alisema kupitia taarifa.
"Matumaini yetu yalikuwa kwamba Rais Trump angechukua hatua zifaazo kuzuia kukiuka Katiba kabla yake kuingia madarakani. Tumelazimishwa kuchukua hatua za kisheria."
Katiba ya Marekani inasema hakuna afisa yeyote wa serikali anayefaa kupokea zawadi au "malipo yoyoye ya kifedha, au ada kutoka kwa serikali ya kigeni.
Mawakili wa Bw Trump wanadai sheria hiyo ni ya kutumiwa tu kuzuia maafisa wa serikali kupokea zawadi au manufaa maalum kutoka kwa nchi za nje na wala si kwa malipo kama vile bili ya hoteli.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment